Mjukuu wa Morgan freeman auwawa

Haki miliki ya picha AP
Image caption Morgan freeman

Mjukuu wa kambo wa nyota wa filamu nchini Marekani Morgan Freeman amedungwa kisu hadi kufa karibu na nyumbani kwake huko New York.

E'Dena Hines alipatikana akiwa na majeraha ya kisu kifuani nje ya nyumba yake katika barabara ya West 162 mapema siku ya jumapili.

Marehemu mwenye umri wa miaka 33 alichukuliwa na ambulansi lakini akatangazwa amefariki katika hospitali ya Harlem.

Lamar Davenport mwenye umri wa miaka 30 kutoka mjini New York alishtakiwa kwa makosa ya mauaji siku ya jumatatu.

Maafisa wa polisi alikuwa na uhusiano wa mapenzi na Hines na alipelekwa katika eneo la mauaji.Pia alichunguzwa hali ya saikolojia yake katika hosptali.

Haki miliki ya picha
Image caption Morgan freeman na mjukuu wake Hines

Hines ni mjukuu wa mke wa kwanza wa Morgan Freeman,Jeanette Adair Bradshaw.

Freeman na Bradshaw walitalakiana mwaka 1979.Freeman alikuwa akimwita mjukuu wake.