Jeshi lapuuza mkanda wa Shekau

Haki miliki ya picha NIGERIA GOVT
Image caption Jeshi lapuuza mkanda wa Shekau

Jeshi la Nigeria limepuuzilia mbali mkanda wa sauti unaodhaniwa ni hotuba ya kiongozi mkuu wa kundi la Boko Haram, Abubakar Shekau, ambaye anasikika akisema kuwa yuko hai na bado ni kiongozi wa kundi hilo.

Msemaji wa jeshi anasema kwamba haijalishi ikiwa Bwana Shekau yuko hai ama amefariki.

Haki miliki ya picha bbc
Image caption Kiongozi wa Boko Harama Abubakar Shekau

Nia kuu anasema ni, wataliangamiza kabisa kundi hilo katika kipindi cha miezi mitatu, kama alivyoamuru Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari.

Juma lililopita Rais wa Chad, Idriss Deby, alisema kuwa Boko Haram limemteua kiongozi mpya, huku tetezi zikitanda kote kuwa Bwana Shekau ameuwawa.