Mashambulizi yalaaniwa Syria

Haki miliki ya picha na
Image caption Raia akiwa amejeruhiwa kwa kile ilichodaiwa na wanaharakati kuwa shambulio la anga lililotekelezwa na vikosi vya Serikali

Mkuu wa Ofisi inayoshughulikia maswala ya kibinaadam ndani ya Umoja wa mataifa, amesema ameshtushwa na mashambulizi yanayoendelea dhidi ya Raia nchini Syria.

Stepen O'Brien amewaambia waandishi wa habari alipotembelea Damascus kuwa kitendo cha kuwalenga raia katika vita hivyo ni kinyume cha sheria, haikubaliki na ni lazima vitendo hivyo vikome.

Alionesha kusikitishwa na mashambulizi ya anga ya vikosi vya Serikali vya siku ya jumapili dhidi ya viunga vya mji wa Damascus vinavyoshikiliwa na waasi

Wanaharakati wamesema siku ya jumatatu kuwa idadi ya waliopoteza maisha kutokana na mashambulizi yaliyotekelezwa katika soko mjini Douma imefikia 96.

Mashambulizi haya yanaelezwa kuwa miongoni mwa mashambulizi yaliyoleta madhara makubwa yaliyojitokeza katika kipindi cha miaka minne cha mgogoro wa Sriyia ambapo mpaka sasa, zaidi ya watu 250,000 wamepoteza maisha.