Zaidi ya watu 20 wameuawa Thailand

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Zaidi ya watu 20 wameuawa Thailand

Mojawepo ya sehemu takatifu na maarufu zaidi katika mji mkuu wa Thailand, Bangkok imelipuliwa na mlipuko mkubwa.

Mwaandishi wa BBC aliyeko mahala pa tukio hilo anasema kuwa takrian watu 20 wamefariki, na wengine wengi wamejeruhiwa huku baadhi yao wakipoteza viungo vyao.

Sauti ya mlipuko huo iliwafanya watu wengi kukimbia huku wakikumbwa na hofu kubwa.

Baadhi yao waliziba barabara na kutatiza pakubwa juhudi za magari ya huduma ya dharura kufikia mahala pa tukio hilo.

Eneo hilo la Erawan Hindu, lililoko mkabala na hoteli moja ya kifahari, pia hutembelewa na maelfu ya wabudha kila siku na ni maarufu sana kwa watalii.

Mwaandishi wa BBC anasema kuwa shambulio kama halo halijawahi kutokea mjini Bangkok.