Muingereza akamatwa Bangladesh kwa mauaji

Image caption Wanablogu wanne wameuwawa kufikia sasa na wanamgambo wenye itikadi kali wa kiislamu nchini Bangladesh

Polisi nchini Bangladesh wamewakamata watu wengine watatu, akiwemo raia mmoja wa Uingereza, kuhusiana na mauwaji ya mwanablogu maarufu ambaye si-mcha Mungu.

Idara ya Polisi inasema kuwa, raia huyo wa Bangladesh mwenye asili ya Uingereza ametajwa kama Touhidur Rahman.

Rahman anashukiwa kutoa ufadhili wa kifedha kwa washukiwa hao wengine wawili waliokamatwa awali.

Haki miliki ya picha Facebook
Image caption Mwanablogu aliyeuawa majuzi Niloy Neel

Washukiwa wawili ambao wanatuhumiwa kuhusika moja kwa moja na mauwaji hayo walikuwa wamekamatwa tayari juma lililopita.

Wahasiriwa wote wawili walikatwa katwa hadi kufa.

Haki miliki ya picha Focus Bangla
Image caption Wanaharakati wa kupigania haki za kibinadamu wameandamana kupinga mauji ya wanablogu nchini Bangladesh

Bwana Rahman anasemekana kuhusika na kundi moja la wanamgambo ambalo limeharamishwa nchini humo- Ansarullah Bangla Team.

Katika miezi michache iliyopita, wanablogu wanne wameuwawa kufikia sasa na kundi linaloshukiwa kuwa la wanamgambo wenye itikadi kali wa kiislamu nchini Bangladesh.