Peremende zenye bangi zauzwa Kenya

Haki miliki ya picha Thinkstock
Image caption Peremende zenye bangi zauzwa Kenya

Wizara ya afya nchini kenya imetoa orodha ya peremende, keki na biskuti bidhaa ambazo inadai zimewekwa bangi.

Katika kile ambacho kinatarajiwa kuwashangaza wazazi, barua ambayo ilitiwa sahihi kwa niaba mahabara ya serikali, ilisema kuwa baadhi ya sampuli 176 zilizochukuliwa kwa peremende maarufu , keki na mandazi zilipatikana zikiwa na bangi baada ya kufanyiwa uchunguzi.

Image caption Peremende zenye bangi zauzwa Kenya

Licha ya watoto kuvipenda bidhaa hizo serikali inataka vipiwe marufuku na kuondolewa kabisa madukani na pia wachuuzi kuzuiwa kiziuza.

Kupitia kwa barua kwenda kwa wakuu wa afya wa kaunti zote 47 nchini Kenya, wizara ya afya imewaamrisha maafisa kukagua maduka yote, maduka ya jumla na sehemu zingine bidha hizo zinaweza kupatikana.