Pistorious kuachiliwa Ijumaa

Haki miliki ya picha AP
Image caption Pistorious kuachiliwa Ijumaa

Mwanariadha mshindi wa nishani ya dhahabu ya Olimpiki katika raidha Oscar Pistorius ataachiliwa kutoka gerezani ijumaa wiki hii.

Mwanariadha huyo raia wa Afrika Kusini alihukumiwa kifungo cha miaka mitano gerezani mwaka uliopita kwa kosa la mauaji ya mpenzi wake bi Reeva Steenkamp katika usiku wa siku ya wapendanao.

Pistorius ametumikia kifungo cha miezi 10 pekee gerezani kati ya miaka mitano ambayo alihukumiwa.

Pistorius anashikilia kuwa alimdhania Steenkamp kuwa ni mwizi alipomfyatulia risasi ndani ya nyumban yake.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Upande wa mashtaka unataka Pistorious aongezewe kifungo

Baada ya kuachiliwa Pistorius anatarajiwa kutumikia muda aliosalia nao katika kifungo cha nyumbani.

Kiongozi wa mashtaka nchini humo anasema kuwa Pistorius alipaswa kufungwa kwa takriban miaka 15 gerezani kwa kusababisha kifo cha mwanamitindo mpenzi wake Reeva Steenkamp.

Chini ya sheria za Afrika Kusini, Pistorius anastahili kufunguliwa kutoka gerezani na kutumikia kifungo cha nyumbani baada ya kutumikia sehemu moja juu ya kumi ya hukumu aliyopewa.

Wakati akitoa hukumu hiyo Jaji Thokozile Masipa alisema kuwa kiongozi wa mashtaka nchini Afrika Kusini alishindwa kuthibitisha kuwa Pistorius alikusudia kuua bi Steenkamp alipofyatua risasi nyumbani kwake.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Wazazi wa bi Steenkamp wamelalamika kuwa muda aliohudumu gerezani hautoshi kumuadhibu kwa kuua mwana wao.

Kwa sasa wakili wa Pistorious ana takriban mwezi mmoja ambao anastahili kukata rufaa kwa ombi la upande wa mashtaka la kutaka mwanariadha huyo aongezewe hukumu yake.

Wazazi wa bi Steenkamp wamenukuliwa wakisema kuwa muda aliohudumu gerezani hautoshi kumuadhibu kwa kuua mwana wao.