Shambulizi la Thailand lalaaniwa

Haki miliki ya picha epa
Image caption Shambulizi la Thailand lalaaniwa

Waziri mkuu wa Thailand ametaja shambulizi la bomu ambalo limewauwa zaidi ya watu ishirini mjini Bangkok hapo jana jumatatu kuwa kisa kibaya zaidi kuwahi kutokea nchini humo.

Prayuth Chan-o-cha amesema kuwa mtu ambaye mienendo yake sio ya kawaida ametambuliwa kwenye picha za kamera za usalama kabla ya mlipuko huo kutokea.

Haki miliki ya picha REUTERS
Image caption Shambulizi la Thailand lalaaniwa

Naye Waziri wa ulinzi nchini Thailand amesema kuwa mlipuko wa bomu uliotokea kwenye makutano ya barabara yenye shughuli nyingi katikati mwa jiji la Bangkok ulilenga kimakusudi wageni wanaozuru taifa hilo kwa nia ya kuvuruga utalii na uchumi wa Thailand.

Bado haijabainika ni nani aliyetekeleza shambulizi hilo lakini mkuu wa majeshi amesema kuwa mbinu zilizotumiwa hazifanani na zile zinazotumiwa na waasi wanaotaka kujitenga kusini mwa taifa hilo.