Karibu watu 60 wauawa Nigeria

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Karibu watu 60 wauawa Nigeria

Ripoti kutoka nchini Nigeria zinasema kuwa karibu watu 60 huenda waliuawa wakati wa shambulizi katika kijiji kimoja kaskazini mashariki mwa nchini lililoendeshwa na watu wanaoshukiwa kuwa wanachama wa na Boko Haram.

Shambulizi hilo lilitokea katika jimbo la Yobe lilifanyika Alhamisi iliyopita na habari hizo zimepatikana kutoka kwa wale walionusurika.

Mwandishi wa BBC nchini Nigeria anasema kuwa ukweli kuwa ilichukua siku tano kabla ya shambulizi hilo kujulikana, ni ishara kuhusu jinsi hali ya usalama ilivyo eneo hilo.

Haki miliki ya picha Nigerian Army
Image caption Karibu watu 60 wauawa Nigeria

Walioshuhudia walisema kuwa wanamgambo wa Boko Haram waliwasili katika kijiji hicho wakitumia pikipiki ambapo walianza kuwafyatulia watu risasi.

Mikakati ya jeshi Nigeria imelidhoofisha kundi la Boko Haram miezi ya hivi majuzi lakini sehemu zingine za kaskazini mashariki mwa Nigeria kama Yobe na jimbo jirani la Borno yako katika hali mbaya kiusalama.