Kuachiliwa kwa Pistorius kumepingwa

Image caption Mwanariadha Oscar pistorius

Waziri wa sheria nchini Afrika Kusini amepinga uamuzi wa kuachiliwa kwa mwanariadha Oscar Pistorius.

Michael Masutha amasema kuwa uamuzi wa kumuachilia mwanariadha huyo umechukuliwa mapema.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Oscar Pistorius na Reeva Steenkamp

Pistorius amekaa gerezani kwa muda wa miezi kumi baada ya kumuua kwa kumpiga risasi mpenziwe Reeva Steenkamp na alitarajiwa kuachiliwa ili atumikie kifungo chake cha nyumami siku ya Ijumaa.