13 wauawa kwenye shambulizi Syria

Haki miliki ya picha no credit
Image caption 13 wauawa kwenye shambulizi Syria

Mshambuliaji wa kujitoa mhanga ambaye alikuwa akiendesha gari lililokuwa limejazwa milipuko ameshambulia vikosi vya jeshi la wakurdi kaskazini mashariki mwa Syria na kuwaua takriban watu 13.

Shirikal la haki za binadamu nchini Syria lenye makao yake nchini Uingereza, linasema kuwa lengo la shambulizi hilo lilikuwa ni kituo cha kijeshi katika mji wa Qamishli.

Kundi la Islamic state limesema kuwa mmoja wa wanamgambo wake aliendesha shambulizi hilo.

Islamic state na vikosi vya wakurdi wamekuwa vikipigana eno hilo kwa miezi kadha.