Picha ya mshambuliaji yatolewa Thailand

Haki miliki ya picha Royal Thai Police
Image caption Picha ya mshambuliaji yatolewa Thailand

Polisi nchini Thailand wametoa picha ya mwanamme aliyevaa fulana ya manjano ambaye anahusishwa na mlipuko ambao uliukumba mjini wa Bangkok siku ya Jumatatu na kuwaua watu 20.

Picha hiyo inaonyesha mwanamme mzungu , mwenye nywele nyeusi ambaye pia alikuwa amavaa miwani.

Haijabainika ikiwa mtu huyo ni raia wa Thailand.

Image caption Picha ya mshambuliaji yatolewa Thailand

Polisi wanaamini kuwa mwanamme huyo hakutekeleza kitendo hicho peke yake lakini bado hawana uhakika kuhusu ni nani aliendesha shambulizi hilo na ni kwa sababu gani.

Eneo lililoshambuliwa limefunguliwa tena na watu wengi wamekuwa wakiwasha ubani , wakiomba na kuweka maua.