Eneo lililoshambuliwa Bangok lafunguliwa

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Eneo lililoshambuliwa Bangok lafunguliwa

Eneo takatifu ambalo lilishambuliwa siku ya Jumatatu katika mji mkuu wa Thailand Bangkok limefunguliwa tena.

Waumini kadha wamekuwa wakiwasha ubani , wakiomba na kuweka maua katika eneo hilo ambapo zaidi ya watu 20 waliuawa.

Sakafu iliyoharibiwa nayo imekarabatiwa tena.

Polisi wanaomtafuta mwanamme ambaye alionekana akitoka eneo kulikotokea shambulizi wamemhoji mmiliki wa teksi ambaye anaaminiwa kumuondoa eneo hilo.

Polisi wanasema kuwa kuna uwezekano kuwa mshukiwa huyo alipelekwa katika uwanja wa ndege.