Uhamiaji:UK na Ufaransa zakubaliana

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Maafisa wa uhamiaji nchini Uingereza

Uingereza na Ufaransa zimetia saini ya makubaliano ya ushirikiano dhidi ya kukabiliana na walanguzi wa wahamiaji.

Mawaziri wa mataifa hayo mawili, walikutana leo katika mji wa Calais ulioko katika bandari ya Ufaransa, mahala ambapo wahamiaji wamekuwa wakijaribu kuvuka na kuingia nchini Uingereza, wakitumia kivukio cha chini kwa chini.

Mataifa hayo pia yamekubaliana kujenga kituo cha usalama ili kuizuia mitandao ya makundi ya walanguzi inayofanya kazi kaskazini mwa Ufaransa.

Sehemu ya makubaliano yaliyotiwa saini na mawaziri hao inajumuisha pia Ufaransa kuongeza opereseheni ya doria katika mpaka huo.

Inakisiwa kuwa kuna wahamiaji wapatao elfu nne ambao wanajaribu kuvuka na kuingia nchini Uingereza kupitia mji huo wa bandari wa Calais.

Hapo jana Jumatano Ujerumani ilisema kuwa inatarajia kuwapokea wahamiaji wapatao laki nane mwaka huu.