Mwanzilishi wa Chama Ufaransa atimuliwa

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Jean Marie le Pen akiwa na mwanawe Marine le pen

Waanzilishi wa Chama cha national front chenye mrengo wa kushoto kimemfukuza mwanzilishi wa chama hicho bwana Jean-Marie Le Pen.

Kuondolewa huko katika nafasi hiyo kubwa kulitokana na ugomvi wake mkubwa na wa waziwazi na mwanae wa kike marine ambae alikichukua chama hicho kutoka kwake miaka minee iliyopita.

Binti yake huyo amekuwa akifanya jitihada za kukinusuru chama hicho kutoka kwenye sura ya ubaguzi wa kirangi na wa dini.

Lakini baba yake alisisitiza chama hicho kiendeleze itikadi zake za awali na kuenzi jadi za chama hicho na kutoa wito hivi karibuni kwa ufaransa kui unga mkono urusi kwa kile walicho kiita kuisaidia dunia ya weupe .

Aliwahi kufanikiwa katika kuweka vizingiti vya kisheria hapo awali vyakumsimamisha kiongozi wa chama hicho.

Na wiki iliyopita bwana le alisema hato mpa kura yake mwanae ifikapo mwaka 2017 katika kugombea nafasi ya uraisi huko nchini ufaransa na kwamba anasikia aibu kutumia jina moja la uko.