Ni nani anayewaua waandishi Sudan Kusini?

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Sudan Kusini

Mauji ya mwandishi wa Sudan Kusini Peter Julius Moi yanajiri wakati ambapo kuna hali ya wasiwasi miongoni mwa waandishi wanaofanya kazi nchini humo.

Takriban waandishi watano wameuawa katika mashambulizi ya kulengwa mwaka huu kulingana na utafiti uliofanywa na kamati ya kuwalinda waandishi CPJ.

Haijulikani ni nani anayehusika ,lakini mauaji hayo yanajiri siku chache tu baada ya CPJ kushtumu matamshi yaliotolewa na rais Salva Kiir wa Sudan kusini.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Salva Kiir

''Uhuru wa vyombo vya habari haumanishi kwamba unahujumu taifa lako.Na iwapo hawajui kwamba taifa hili limeua watu,tutawaonyesha siku moja'',aliwaambia waandishi katika mji wa juba siku ya jumapili.