Serikali ya Zimbabwe yategemea wahubiri

Image caption Waziri wa afya kushoto akipokea dola 120,000 kutoka kwa muhubiri Walter Magaya

Serikali ya Zimbabwe inaendelea kukabiliwa na matatizo katika kuafikia malengo yake ya kifedha, kwa hivyo imeanza kuwategemea wahubiri maarufu wanaojitambulisha kama manabii .

Siku ya alhamisi waziri wa afya David Parirenyatwa alipokea takriban dola 120,000 kutoka kwa Walter Magaya wa kanisa la PHD,ili kukarabati vituo vya afya.

Kwa sababu ya hali mbaya za kiuchumi,miujiza huvutia raia wengi na hivyobasi kuchangisha fedha nyingi kila jumapili.