Lubanga:'Nataka kusomea chanzo cha ukabila'

Haki miliki ya picha AP
Image caption Lubanga

Mtu wa kwanza kabisa kuhukumiwa na mahakama ya kimataifa ya makosa ya Jinai iliyoko the Hague nchini Uholanzi, ameiambia mahakam hiyo kuwa anataka kurejea nyumbani ili kusomea chanzo cha mapigano ya kikabila.

Mbabe huyo wa kivita raia wa Congo, Thomas Lubanga, alisema hayo wakati wa kusikizwa kwa kesi yake, ambapo majaji wanajaribu kuona iwapo anaweza kufunguliwa mapema baada ya kuhudumia robo tatu ya kifungo chake.

Ameiambia mahakama hiyo ya ICC kuwa, amegundua uwezo wake mkubwa alio nao wa kuleta uwelewano na upatanishi nchini DRC.

Bwana Lubanga anahudumia jela miaka kumi na nne kwa kuwatumia watoto kama wanajeshi katika vita na makosa mengine.

Amekuwa kifungoni tangu mwaka 2006.