Ugiriki:Waasi wa Syriza kubuni chama

Haki miliki ya picha AP
Image caption Alexi Tsipras

Siku moja baada ya waziri mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras, ambaye pia ni mwanachama wa chama cha mrengo wa kushoto kutangaza kujiuzulu kwake, hatua hiyo imechochea uwezekano wa kufanyika kwa uchaguzi mkuu.

Wabunge 25 kutoka katika chama chake cha Syriza, wanasema kwamba wanajiondoa na kuunda chama kingine kipya.

Kundi hilo linaongozwa na waziri wa zamani wa kawi, ambaye amekuwa katika mstari wa mbele kukosoa hatua za Bwana Tsipras kuhusiana na masharti ya madeni ya Ugiriki kutoka kwa wakopeshaji wake.

Rais wa Ugiriki amekipa chama kikuu cha upinzani cha conservative kiitwacho New Democracy, siku tatu kuunda serikali mpya ya muungano wa kitaifa.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Ugiriki

Kiongozi wa chama hicho, Vangelis Meimarakis, amesema kwamba atajaribu kufanya hivyo ili kuzuia uwezekano wa kufanyika kwa uchaguzi wa mapema.

Mwaandishi wa BBC, anasema kuwa hakuna chama kingine kitakachoweza kupata idadi inayohitajika bungeni kubuni serikali, ni bayana kuwa uchaguzi mkuu mwingine utaitishwa.

Bwana Tsipras amesema kuwa anajiuzulu kuwaruhusu wapiga kura kutoa kauli yao kuhusiana na mkopo ambao ugiriki itapokea kutoka kwa mataifa ya Ulaya kuukwamua uchumi wake.