Miezi 6 jela kwa wapenzi wa jinsia moja

Haki miliki ya picha
Image caption Watu 7 wamehukumiwa kifungo cha miezi sita jela kwa kuenda kinyume na madili.

Watu 7 wamehukumiwa kifungo cha miezi sita jela kwa kuenda kinyume na madili.

Watu hao walipatikana na hatia katika mahakama moja ya Senegal kwa kushiriki ngono na watu wa jinsia yao.

Mahakama mjini Dakar ilielezwa kuwa wanaume hao walinaswa katika mtego uliowekwa na maafisa wa Polisi katika makazi ya mmoja wao.

Mama mzazi wa mmoja wa watuhumiwa alikiri kuwa mwanawe alikuwa na mpenzi wa jinsia yake japo alikataa kufika mahakamani kutoa ushahidi.

Ngono ya wapenzi wa jinsia moja ni haramu nchini Senegal.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Obama aliitaka Kenya iwaache huru wapenzi wa jinsia moja lakini ombi lake likakataliwa na rais Kenyatta

Wanaopatikana na hatia ya kushiriki mapenzi ya jinsia moja wanaweza kufungwa hadi miaka mitano gerezani na faini ya takriban dola elfu mbili na mia tano (2500).

Wakili wa washtakiwa Abdoul Daff alisema kutokuwepo kwa mashahidi bila shaka kulimaanisha kuwa upande wa mashtaka haukuwa na ushahidi wa kutosha na hivyo kesi hiyo ingesambaratika.

'Ikiwa hakuna mashahidi basi hakuna kesi 'alisema bwana Daff.

je ni wapi ambapo ni haramu kuwa na mpenzi wa jinsia moja ?

''nafikiri kwa sasa tutaenda zetu tukae na kufikiria kwa kina kisha tutapanga upy tutakachokifanya'' ,aliongezea wakili huyo

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mapenzi ya jinsia moja ni haramu katika mataifa 38 barani Afrika.

Asilimia 95 % ya wasenegal ni waislamu na watu wenye wapenzi wa jinsia moja hulazimika kuweka penzi lao kuwasiri kubwa.

Hata hivyo mwanaharakati wa kupigania haki za wapenzi wa jinsia moja

Djamil Bangoura amepinga vikali kauli ya mahakama hiyo.

''Inasikitisha kuona wanaume wa Senegal wakihukumiwa kwa kuwa na wapenzi wa jinsia moja''.

Haki miliki ya picha Isaac Kasamani l AFPl Getty
Image caption Unaweza kuhukumiwa kifo iwapo utapatikana ukishiriki mapenzi ya jinsia moja nchini Sudan, Mauritania, Somalia na Nigeria.

katika ziara yake nchini Kenya mwezi uliopita rais wa Marekani Barack Obama aliomba mataifa ya Afrika yawaweke huru watu wenye wapenzi ya jinsia moja.

Ombi lake lilikataliwa wazi na mwenyeji wake rais Uhuru Kenyatta.

Mapenzi ya jinsia moja ni haramu katika mataifa 38 barani Afrika.

Unaweza kuhukumiwa kifo iwapo utapatikana ukishiriki mapenzi ya jinsia moja nchini Sudan, Mauritania, Somalia na Nigeria.