Korea Kaskazini yaitishia Korea Kusini

Haki miliki ya picha YONHAP AFP
Image caption Korea Kaskazini yaitishia Korea Kusini

Huku msukosuko ukiendelea kushuhudiwa katika rasi ya Korea, Korea kusini inasema kuwa Korea Kaskazini imepeleka silaha kwenda kwa mpaka baada ya kutoa vitisho vya kuharibu vipasa sauti vinavyotangaza propaganda kutoka Korea kusini.

Muda wa mwisho uliotangazwa na Korea Kaskazini wa kutaka kuondolewa kwa vipasa sauti hivyo unatarawajiwa kukamilika saa chache zinazokuja,

Haki miliki ya picha
Image caption Vipasa sauti vya Korea Kusini

Korea Kusini inasema kuwa itajibu vikali . Ndege zake za kivita zimekuwa zikiruka pamoja na za Marekani karibu na mpaka.

Mwandishi wa BBC nchini Korea Kusini anasema kuwa ni muda uliotangazwa na korea kaskazini ndio unaoifanya hali kuwa hatari zaidi.