Iran yasifu uhusiano na Uingereza kurudi

Waziri wa UIngereza, akifungua tena ubalozi wa  nchi yake mjini Teheran Haki miliki ya picha bbc

Iran imesifu awamu mpya katika uhusiano wake na Uingereza baada ya nchi zote mbili kufungua tena ofisi zao za ubalozi.

Waziri wa mashauri ya nchi za nje wa Iran, Javad Zarif, amesema baada ya misukosuko msingi wa uhusiano sasa ni kuheshimiana.

Kufunguliwa tena kwa ubalozi wa Uingereza mjini Tehran, miaka mine baada ya kuvamiwa na waandamanaji, kunaonesha kuwa uhusiano na mataifa ya magharibi umetengenea tangu mkataba wa nuklia wa kimataifa kutiwa saini mwezi uliopita.

Lakini mwandishi wa BBC katika seherehe ya ufunguzi wa ubalozi wa Uingereza, anasema kwa Wairan wengi, ubalozi huo ni alama ya siasa za Uingereza kuingilia kati ya mambo ya nchi yao.