Wahamiaji wawasili Serbia

Wahamiaji waliponasa kwenye mpaka wa Ugiriki na Macedonia Haki miliki ya picha bbc

Maelfu ya wahamiaji wamejaa pomoni kwenye kituo cha mapokezi nchini Serbia, wakiendelea na safari yao kuelekea nchi za Umoja wa Ulaya.

Waziri wa ulinzi wa Serbia, Bratislav Gasic, alizuru kituo hicho na alisema polisi wanafanya kazi saa zote kutoa vibali vinavyoruhusu wahamiaji hao kupita Serbia.

Wahamiaji hao walisafiri kwa mabasi na treni kupita Macedonia, baada ya nchi hiyo kuacha kuwazuwia mpakani.

Mashirika ya kutetea haki za kibinaadamu yalilaani hatua ya wakuu wa Macedonia baada ya wahamiaji, wengi wao kutoka Syria, walipoachwa nje bila ya hifadhi wakati wanazozana na polisi mpakani.