Ban Ki Moon ziarani Nigeria

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon amewasili jana nchini Nigeria kuanza ziara ya siku mbili.

Anaitembelea Nigeria kwa lengo kuwatembelea waathirika wa mashambulizi yaliyofanywa katika ofisi za umoja huo mjini Abuja yanayodaiwa kufanywa na wanamgambo wa Boko Haram miaka minne iliyopita. Ban Ki Moon pia atakutana na Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari kujadili namna ya kupambana na vikundi vyenye msimamo mkali.

Anatarajiwa pia kuwa na mazungumzo na makundi yanayoendesha kampeni za kuwarudisha wasichana wa shule zaidi ya mia mbili waliotekwa na Boko Haram mwaka uliopita.