Je, wajua maji ni adui kwa baadhi ya Wachina?

Image caption Edwin Mmari kushoto kutoka Tanzania ni miongoni mwa Waafrika waliowaopa Wachina

Je, una habari maji ni adui mkubwa kwa baadhi ya Wachina? Katika mazungumzo yangu na raia kutoka Afrika wanaoishi hapa Beijing wananieleza wenyeji hawatilii maanani sana kuoga kila siku, na wengine nyumba zao zimejengwa bila bafu hivyo basi inawalazimu watafute sehemu ya nje ya kuogea.

Alice Achieng ambaye amefanya kazi hapa kwa miaka saba na Ramadhani Pondamali wananieleza hapo mwanzo walishangazwa sana na tabia hiyo lakini sasa imebidi wazoee.

Asema Achieng:''Kila siku nilikua naskia hawa Wachina tunafanya nao kazi wanatoa uvundo ambao si wa kawaida ndio nikauliza wenzangu kutoka Kenya na Tanzania tunaofanya nao kazi hapa, wakaniambia ni kwa sababu ya kutooga.''

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Beijing Uchina

''Duh, mimi yaani sikuamini kabisa siku za mwanzo,'' asema Pondamali.''Iweje mtu mzima na akili zako ukose kuoga uingie ofisini na harufu hiyo ya kusinya.''

Ni kwa nini hawapendi kuoga?, Achieng anasema ni kama tabia yao tu hata kusugua meno asubuhi wengine wao ninaelezwa hawafanyi hivyo.

''Utasikia tu mtu anatoa harufu mbaya mdomoni, sasa unashindwa kazi rahisi kama hiyo inawashindaje tena ni usafi wako binafsi.

Image caption Fatma Halnur ni mchina anayezungumza kiswahili.Ni mwanafunzi katika chuo cha Lugha za wageni cha Beijing.

''Ni tabia mbaya sana kusema ukweli. Lakini hatuwezi kuwauliza wajua tuko ugenini lazima tuzoee tabia za wenyeji wetu na tuchunge unga wetu.''

Hata wanafunzi wa Kichina pia wana hiyo tabia. Maji ni adui mkubwa kama nilivyoelezwa na wanafunzi kutoka Afrika.

Mbali na uadui wao na maji, Wachina ama kwa hakika wamepiga hatua kubwa kwa upande wa uchukuzi hasa magari ya abiria kwani kuna mabasi makubwa na treni za chini ya ardhi zinazozingatia sana muda wa kazi.

Hapo serikali ya China imejaribu sana, na inastahili kuigwa na mataifa wanayofanya nayo biashara kama vile Kenya, Tanzania na Zambia.

Image caption Sekta ya Uchukuzi nchini Uchina imeimarika zaidi

Na kama watoka Afrika ukiwa hapa itabidi uzoee kuangaliwa kwa muda mrefu na Wachina ambao wanaona ajabu sana kukutana na Wafrika mpaka wengine anasugua ngozi waone kama itatoka, na wengine watakuomba upige picha nao huku wakicheka na kufurahia kukuona.

Baadhi yao wanachukulia Wafrika wako nyuma sana kiasi kwamba wengine hutema mate kwa dharau wakikutana na Mwafrika.

Lakini kwa upande wangu nakaza macho na kuwaangalia bila wasiwasi kwa sababu naelewa si makosa yao.

Ni ukosefu wa elimu kuhusu mataifa mengine ya nje. Wao Wachina wanaamini sana nchi yao na ni wazalendo wa hali ya juu.

Haki miliki ya picha z
Image caption Beijing Uchina

Nitazidi kukudondolea mengi kuhusu China nikiwa hapa Beijing kwa mashindano ya dunia ya riadha..