Misururu yashuhudiwa hospitalini Ghana

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Ghana

Kuna misururu mirefu katika kitengo cha wagonjwa wanaokwenda katika hospitali za serikali ya Ghana ,baada ya madaktari kurudi kazini kufuatia mgomo wa wiki tatu.

Mazungumzo kati ya serikali na chama cha wahudumu wa sekta ya afya yanatarajiwa kuendelea baadaye hii leo.

Madaktari wanapigania elimu ya bure,marupurupu bora,kuongezewa mavazi,na marupurupu ya mafuta pamoja na yale ya kuwadumisha.

Serikali hadi kufikia sasa imekataa kukubali matakwa yao.