Korea kupunguza hali ya wasiwasi mpakani

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Korea kaskazini na kusini

Korea kaskazini na Kusini zimefikia makubaliano ya kupunguza hali ya wasiwasi iliyopo mpakani mwa nchi hizo mbili.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya mazungumzo ya muda mrefu.

Nchi zote mbili ziliweka vikosi vyake vya ulinzi kama tahadhari baada ya mapigano ya muda mfupi yaliyotokea wiki iliyopita.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na pande zote mbili, Korea kusini imekubali kuacha kueneza habari zenye propaganda zinazochochea pande mbili hizo, huku Korea kaskazini ikielezea masikitiko yake juu ya tukio la hivi karibuni la utegaji bomu lililojeruhi wanajeshi wawili wa Korea kusini.

Nchi hizo mbili pia zimekubaliana kufanya tena mazungumzo ya kuimarisha uhusiano wao.