Washukiwa 14 wa 'Islamic state' wakamatwa

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wapiganaji wa Islamic state

Uhispania na Morocco zimewatia mbaroni watu 14 katika operesheni ya pamoja, iliyowalenga washukiwa wanaoandikishwa kujiunga na kundi la wanamgambo wa Islamic State.

Washukiwa hao ambao wamezuiliwa walikamatwa nje ya mji wa Madrid na maneo mbalimbali ya Morocco.

Mnamo Ijumaa iliyopita, Ayoub El-Khazzani mwenye umri wa miaka 25 raia wa Morocco, ambaye ameishi nchini Uhispania kwa miaka saba, alikamatwa baada ya shambulio ndani ya treni kutibuliwa.

Ayoub El-Khazzani mwenye umri miaka 25 kutoka eneo la Tetouan kaskazini mwa Morrocco aliwasili nchini Uhispania mwaka 2007 na kuishi eneo hilo kwa miaka saba katika miji ya Madrid na Algeciras kabla ya kuelekea nchini Ufaransa.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ayoub El Khazzani

Anatuhumiwa kuwasiliana na waislamu wenye itikadi kali na tayari alikuwa ameorodheshwa kama mtu hatari na mamlaka ya Uhispania.

Mnamo mwezi Februari Uhispania ilielezea Ufanransa kuhusu wasiwasi wao.