Mugabe azomewa na wapinzani

Haki miliki ya picha AP
Image caption Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amezomewa na wabunge wa upinzani alipokuwa anahutubia nchi kupitia bunge la nchi hiyo.

Wakati wa hotuba hiyo kulikua na kelele za wabunge kiasi cha sauti ya kiongozi huyo kutosikika vizuri.

Wabunge hao wanadai kuwa hakukua na jipya katika mipango aliyoeleza Rais Mugabe kuisaidia nchi hiyo kuondoka katika mgogoro wa kiuchumi unaoukabili.

Pia waliimba nyimbo kuhusu chama tawala nchini humo kupoteza mvuto.

Wabunge wa chama tawala cha ZANU-PF walijibu kwa kuimba kuwa kiongozi huyo mwenye miaka tisini na moja ataendelea kuwa madarakani.

Hotuba yake iliisha kwa kipindi cha chini ya nusu saa,ni miongoni mwa hotuba fupi sana kuwahi kutolewa na kiongozi huyo.