Soko huru kudhibiti viwango vya Rand

Image caption Sarafu ya Rand

Benki kuu ya Afrika Kusini imesema kuwa soko huru la nchi hiyo litaendelea kuruhusu soko kuweka viwango vya sarafu ya rand.

Benki hiyo ilikuwa inajibu kuporomoka kwa thamani ya sarafu hiyo baada ya kuanguka kwa kiwango cha chini zaidi ikilinganishwa na sarafu ya dola siku ya jumatatu.

Benki hiyo imesema kuwa ijapokuwa ina wasiwasi kuhusu msukosuko haitabadili sera zake,hatahivyo haijapinga kuingilia kati iwapo kuna tishio la utendaji wa masoko.

Hatahivyo thamani ya sarafu hiyo ilipanda kiasia jumanne asubuhi.