Uingereza na uhamiaji haramu

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Polisi wa Uingereza akimdhibiti mhamiaji haramu

Serikali ya Uingereza itatangaza leo Jumanne mapendekezo mapya ya kukabiliana na suala tata la uhamiaji.

Wahamiaji ambao watapatikana wakifanya kazi kinyume na sheria nchini Uingereza na Wales, watakabiliawa na hukumu ya hadi miezi sita gerezani na kupigwa faini ya fedha nyingi.