Waethiopia na Wakenya wafuzu mita 5,000

Image caption Mbio za mita 5000

Wanariadha 3 wa Ethiopia pamoja na wengine 3 wa Kenya wamefuzu katika fainali ya mbio za mita 5000 siku ya jumamosi mjini Beijing.

Wanariadha hao ni pomoja na Yomif Kejelcha ambaye ana mda bora mwaka 2015 kufikia sasa.

Vilevile wanaraidha ambao wamefuzu kukabiliana na bingwa mtetezi wa mbio hizo kutoka Uingereza Mo Farah ni Imane Merga na Hagos Gebrhiwet wa Ethiopia pamoja na Wakenya Edwin Soi,Caleb Ndiku na Isiah Koech.

Farah ambaye analenga kupata medali ya pili ya mashindano hayo alijibiidisha na kumaliza miongoni mwa wale waliofuzu baada ya kutegwa wakati alipokuwa akikimbia.