Marekani yamuonya rais Salva Kirr

Image caption Salva Kiir

Marekani imemuonya rais wa Sudan Kusini Salva Kirr, kuheshimu na kutekeleza mkataba wa amani aliousaini siku ya Jumatano mjini Juba.

Rais Kirr, alikuwa amekataa kusaini mkataba huo wiki iliyopita mjini Adis Ababa Ethiopia.

Lakini, licha ya kusaini mkataba huo, ameelezea wasi wasi wake kuhusiana na masuala kadhaa ya mkataba huo, hasa kugawana madaraka na waasi.

Mkataba huo unanuiwa kumaliza mzozo uliodumu kwa muda wa miezi Ishirini.

Usitishwaji wa mapigano unapaswa kutekelezwa katika muda wa saa 24 na majeshi ya kigeni yanapaswa kuondoka nchini humo.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Sudan Kusini

Hakuna wanajeshi watakaoruhusiwa kufika karibu na mji mkuu Juba.

Kiir ambaye alikabiliwa na shinikizo za kimataifa kuidhinisha mkataba huo anatarajiwa kuunda serikali ya umoja wa kitaifa na kiongozi wa waasi Riek Machar.