Syria ina imani na washirika wake

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Rais Bashar al Assad

Rais Bashar al-Assad, amesema ana imani licha ya tuhuma kwamba Iran na Urusi huenda zikamtenga kutoa nafasi ya makubaliano kufuatia makubaliano ya nyuklia ya Iran na mataifa ya magharibi.

Licha ya shughuli nyingi za kidiplomasia katika eneo hilo kufuatia makubaliano hayo, Assad amesema hakuna dalili ya makubaliano ndani ya Syria, na amemshutumu mumbe maalum wa kimataifa wa amani kwa kuwa na upendeleo.

Katika mahojiano marefu na yasiokuwana ushindani, katika kituo cha televisheni cha Lebanon - al Manar inayoendeshwa na washirika wake wa Hezbollah, Rais Assad alitaja nafasi zilizopo ambazo hazijabadilika licha ya hali duni inayovikabili vikosi vyake katika vita.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Raia wengi wameathirika na ghasia na mapigano Syria

Jitihada za kidiplomasia zimeshinikizwa baada ya makubaliano hayo na Iran ya nyuklia, na kusababisha uvumi kwamba huenda kukawa na muafaka wa Syria.

Lakini rais Assad amesema kwamba hakuna uwezekano wa kufikiwa suluhu.Na ili hilo liweze kufanyika, basi wale aliowataja kuunga mkono "ugaidi" - akimaanisha Saudia Waturuki na wengine - itabidi wasite kufanya hivyo.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption watu 250,000 wamefariki katika mzozo huo

Suluhu yoyote ni lazima itokane kwanza na vita dhidi ya ugaidi.

Ameeleza imani yake kwa Urusi na Iran ambao amezitaja nchi hizo kutowatenga rafiki zake tofauti na Marekani.

Na iwapo Iran itaibuka na nguvu zaidi kutokana na makubaliano ya nyuklia, amesema hilo litakuwa na faida kwa washirika wake Syria.