Msichana wa miaka 16 akiri kuwa gaidi

Image caption Mahakama ya manchester

Msichana mmoja wa miaka 16 amekiri kutekeleza ugaidi katika mahakama moja ya mjini Manchester Uingereza.

Msichana huyo ambaye jina lake haliwezi kutajwa amekiri kumiliki vilipuzi na maelezo ya kutengeza bomu.

Kukamatwa kwake mnamo mwezi Aprili kunafuatia uchunguzi na kitengo cha kukabiliana na ugaidi cha kaskazini magharibi.

Alikamatwa pamoja na mvulana mmoja wa miaka 14 kutoka eneo la Blackburn ambaye amekiri kuhusika katika njama ya kuwashambulia polisi katika gwaride nchini Australia.

Msichana huyo alikiri mashtaka mawili ya kumiliki stakhabadhi zilizo na habari zinazoweza kumsaidia kutekeleza kitendo cha ugaidi.

Alituhumiwa kumiliki nakala zenye maelezo ya kutengeza bomu ya kitabu cha Anarchist CookBook.