Wahamiaji 50, wafariki Libya

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Wahamiaji haramu

Watu wapatao 50 wamekutwa wamekufa ndani ya boti iliyokuwa imebeba wahamiaji waliokamatwa katika pwani ya Libya.

Maiti za watu hao zilikutwa katika sehemu ya mizigo ya boti hiyo.

Vyombo vya habari vya Italia vimesem kwamba vifo hivyo vinaweza kuwa vimesababishwa na kukosa hewa.

Kiasi cha watu 430 waliokolewa wakiwa hai kutoka katika boti hiyo na boti ya ulinzi ya Sweden.