Mamia wahofiwa kufa maji Libya

Zoezi la uokoaji zinaendelea katika pwani ya Libya baada ya boti mbili zilizokuwa na zaidi ya wahamiaji 500 kuzama karibu na bandari ya Zuwara.

Watu zaidi ya ishirini na moja wameokolewa lakini mamia ya watu hawajulikani walipo wakihofiwa kufariki dunia.

Taarifa ambazo hazijathibitishwa zinasema kuna zaidi ya miili miamoja katika hospitali ya Zuwara, wakiwemo raia wa Syria, Bangaladesh na nchi kadhaa za Afrika katika jangwa la Sahara.

Hadi sasa kwa mwaka huu pekee,zaidi ya wahamiaji elfu mbili wamefariki wakijaribu kuvuka kutoka Libya kwenda Italia kwa boti ambazo sio salama ndani ya maji.