Man U yasonga mbele UEFA

Image caption Wachezaji wa Manchester United wakifurahi

Katika muendelezo wa mechi za mkondo wa pili kufuzu kwenye mashindano ya klabu bingwa barani Ulaya, usiku wa kuamkia leo timu kadhaa zilishuka dimbani kutafuta tiketi ya kuingia katika hatua ya makundi.

Manchester Utd imefanikiwa kusonga mbele kwa kishindo baada ya kuibuka na ushindi wa bao 4-0 dhidi ya Club Brugge na kufanya matokeo kuwa 7-1, katika mikondo yote miwili.

Katika mchezo huo nahodha Wayne Rooney alidhihirisha kuwa bado yupo vizuri katika kucheka na nyavu, baada kufunga mara tatu.

Droo ya makundi ya ligi hiyo, inatarajiwa kufanyika leo hii.