Lamorde akanusha madai ya ufisadi

Ibrahim Lamorde
Image caption Mkurugenzi wa tume ya kupambana na ufisadi Nigeria

Mkurugenzi mkuu wa shirika la kupambana na ufisadi nchini Nigeria, Ibrahim Lamorde amekanusha madai kuwa zaidi ya dola bilioni tano zimetoweka kutoka kwa hazina ya shirika hilo.

Kamati ya Bunge la Senate, inayochunguza madai kuwa mali ya fedha zilizofichuliwa na tume ya kupambana na uhalifu wa kiuchumi nchini humo EFCC, zilikuwa zimepelekwa kwingineko.

Bwana Lamorde ameiambia BBC kuwa madai hayo hayana msingi na yananuiwa kumharibia sifa, kwa sababu tumu hiyo ya EFCC kwa sasa inamchunguza mtu aliyetoa madai hayo.

Seneta Peter Nwaoboshi, ambaye anaongoza uchunguzi huo, alifahamishwa madai hayona George Uboh, ambaye ni mtaalamu wa masuala ya ulinzi.

Bwana Uboh kwa sasa anakabiliwa na mashtaka ya kuiba mali ya serikali, madai ambayo ameyakanusha.

Lakini Lamorde amesema, hata fedha zilizokusanywa na tume ya EFCC zikijumuishwa na ufadhili wote, unaotolewa na shirika hilo, haviwezi kufika dola bilioni tano kwa pamoja.