Wahamiaji 71 waangamia ndani ya Lori Austria

Haki miliki ya picha 4 news
Image caption Lori lililokuwa na miili ya wahamiaji

Maafisa wa polisi nchini Austria, wamethibitisha kuwa miili ya wahamiaji 71, imepatikana ndani ya lori moja iliyokuwa imeachwa kwenye barabara kuu.

Miili hiyo inajumuisha 59 ya wanaume, 8 ya wanawake na watoto wanne.

Msemaji wa polisi amesema kuwa wao wanashuku kuwa wahamiaji hao wanatoka nchini Syria.

Ameongeza kuwa watu watatu wamekamata nchini humo kuhusiana na vifo hivyo.

Wawili kati yao wakisiwa kuwa raia wa Bulgaria na mwiinge ni raia wa Bulgaria mwenye asili ya Lebabon

Waziri wa masuala ya ndani amesema tukio hilo linaashiria umuhimu wa suala la uhamiaji kushughulikiwa kwa dharura na viongozi wa Muungano wa Ulaya EU.

Miili hiyo imepatikana wakati viongozi wa Ujerumani ,Austria na nchi sita za mashariki mwa visiwa vya Balkan, wakikutana mjini Vienna kuzungumzia tatizo la uhamiaji.

Kansella wa Ujerumani Angela Merkel, amesema viongozi hao wamesikitishwa na ripoti hiyo.

Haki miliki ya picha
Image caption Kambi ya wahamiaji Austria

Amesema tukio hilo ni onyo kwa mataifa ya Ulaya kwamba swala la uhamiaji linaweza tu kutatuliwa iwapo kutakuwa na ushirikiano na uwajibikaji.

Nchi za ulaya zinazopokea idadi kubwa wahamiaji zimeonya kuwa iwapo nchi zingine hazitakubali kuwapa hifadhi wahamiaji athari za haua hiyo zitashuhudiwa katika Jumuiya nzima ya Ulaya.