Camara azuiwaa kurudi nyumbani-Guinea

Image caption Moussa Dadis Camara

Aliyekuwa kiongozi wa kijeshi nchini Guinea, anayeishi uhamishoni, Moussa Dadis Camara ameiambia BBC kuwa utawala wa nchi hiyo unamzuia kurejea nyumbani.

Kiongozi huyo wa kijeshi alikuwa akirejea nyumbani kupitia mji mkuu wa Ivory Coast, Conakry siku ya Jumatano, lakini ndege alimokuwa akisafiria, ilinyimwa idhini ya kutua mjini Abidjan na ililazimika kurejea Ivory Coast.

Camara amesema anadhani rais wa Guinea Alpha Conde hataki arejea nyumbani kwa sababu agizo la kutoruhusu ndege hiyo kutua ilitoka mjini Conakry.

Kapteni Camara anatarajia kurejea nyumbani ili awanie kiti cha urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu, lakini pia anasakwa kuhusiana na mauaji ya watu 150, katika uwanja mmoja wa michezo katika mji mkuu wa Guinea mwaka wa 2009