Vyuo vikuu Ghana vyahusishwa na IS

Image caption Mwanafunzi wa chuo kikuu Ghana

Serikali ya Ghana imeanzisha uchunguzi kuhusiana na madai kuwa vyuo vikuu nchini humo vimetumika kama vituo vya kuwasajili wapiganaji wa Islamic State.

Mratibu wa masuala ya usalama nchini humo Yaw Donkor amesema kuwa kundi hilo la IS limekuwa likiwasajili wanafunzi baada ya kuwahimiza kwenye mitandao ya Internet.

Donko amethibitisha kuwa raia wawili wa nchi hiyo ambao wamesafiri kujiunga na kundi hilo.

Kundi hilo la Kiislamu, linalojulikana kwa ukatili wake kwa sasa inathibiti maeneo kadhaa ya Iraq and Syria.