Watuhumiwa vifo Austria kortini

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Lori linalodaiwa kuwa na miili ya wahamiaji walikutwa wamekufa

Watu wanne waliotiwa mbaroni baada ya miili ya watu sabini moja ya wahamiaji kupatikana kwenye lori nchini Austria wanatarajiwa kufikishwa mahakamani nchini Hungary leo.

Watuhumiwa hao wanne raia watatu Bulgaria mmoja raia wa Afghanstan akiwemo mmiliki wa gari na madereva wawili.

Timu ya wataalamu wa utambuzi mjini Viena wanaendelea kufanya uchunguzi wa baadhi ya miili na wengine wanawasili kutoka katika magari yenye jokovu kutokea Nickelsdorf mahali ambapo gari lililokuwa na miili lilipogundulika.

Waliokufa ni pamoja na watoto wadogo wenye umri chini ya miaka miwili.

Inasadikiwa waliokufa walitokea nchini Syria.