71 wafa Austria,mshukiwa wa 5 akamatwa

Haki miliki ya picha bb
Image caption Lori lililotumika kusafirisha wahamiaji

Polisi nchini Hungary wamemkamata mtu wa tano kufuatia vifo vya wahamiaji 71 waliopatikana ndani ya lori moja wiki iliyopita.

Wanasema kuwa wanamchunguza mwanamme huyo ambaye ni raia wa Bulgaria kwa kushukiwa kuhusika kwenye usafirishaji haramu wa watu.

Gari hilo lilipatikana limeachwa kwenye barabara moja nchini Austria. Raia watatu wa Bulgaria na mmoja kutoka Afghanistan wamekamatwa.