Wahamiaji watachukuliwa alama za vidole

Wahamiaji Utaliana Haki miliki ya picha AZZARO AFP

Mawaziri wa mambo ya ndani ya nchi wa Ufaransa, Ujerumani na Uingereza wametoa wito kwamba viwekwe vituo vya kupokea wahamiaji huko Ugiriki na Utaliana, kuhakikisha kuwa wahamiaji wanaandikishwa na alama za vidole kuchukuliwa wanapowasili Ulaya.

Piya wamesema Umoja wa Ulaya unafaa kuwa na orodha ya zile zilizoitwa "nchi salama" ambako wahamiaji wanatoka - ili baadhi ya wahamiaji warejeshwe makwao haraka.

Hapo awali waziri wa mashauri ya nchi za nje wa Ufaransa, Laurent Fabius, ameelezea msimamo wa baadhi ya nchi za Umoja wa Ulaya katika tatizo la wahamiaji kuwa msimamo wa aibu; na alilaani baadhi ya wanachama wa Umoja wa Ulaya kwa kukataa kupokea wakimbizi.

Mkutano wa mawaziri wa Umoja wa Ulaya utafanywa katika wiki mbili zijazo kujadili tatizo hilo la wahamiaji wanaozidi kuongezeka.