Bashir kusafiri kwenda China

Haki miliki ya picha AP
Image caption Rais Omar Al-Bashir

Rais wa Sudan Omar al-Bashir anatarajiwa kusafiri kwenda nchini China kwa ziara ya siku nne, na kupuuza waranti wa kakamatwa ambao ulitangazwa dhidi yake na mahakama ya kimataifa ya ICC.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Sudan ni kuwa rais Al-Bashir anatarajiwa kushiriki katika sherehe za kuadhimisha miaka 70 ya kumalizika kwa vita vya pili vya dunia na kufanya mazungumzo na maafisa wa China kuhusu masuala ya ushirikiano wa kiuchumi.

Haki miliki ya picha g
Image caption Mahakama ya ICC

Mahakama ya ICC ilitangaza waranti wa kukamatwa kwa rais Al-Bashir mwaka 2009 na mwaka 2010, baada ya kumshutumu kwa kuendesha uhalifu wakati alipokuwa akikabiliana na uasi katika eneo la Magharibi la Darfur.

Mwezi Juni mwaka huu Bashir alitishiwa kukamatwa nchini Afrika Kusini wakati mahakama moja ilizuia asiondoke nchini humo baada ya shirika moja lisilo la kiserikali kuwasilisha kesi ya kutaka akamatwe.