Boko Haram yadaiwa kuenea hadi Lagos

Haki miliki ya picha Nigerian Army
Image caption Jeshi la Nigeria

Maafisa wa serikali nchini Nigeria wamesema kuwa kundi la wapiganaji wa Kiislamu wa Boko Haram, wanajaribu kupanua shughuli zao kutoka maeneo ya Kaskazini, yenye idadi kubwa ya Waislamu, hadi mji mkuu wa Lagos na maeneo mengine.

Wakakti huo huo idara ya ujasusi nchini humo imesema kuwa imewakamata takriban makamanda 20 wa kundi hilo la Boko Haram.

Aidha idara hiyo imesema kuwa wapiganaji wengine wamekamatwa katika majimbo yaliyo Kaskazini mwa nchi ya Kano, Gombe , Central Plateau, pamoja na maeneo ya Lagos Kusini na Enugu kati ya Julai na Agosti mwaka huu.

Haki miliki ya picha Boko Haram Video
Image caption Boko Haram

Taarifa hiyo kutoka kwa idara ya huduma za kitaifa inasema kuwa wapiganaji hao wa Boko Haram wameanza kuhamahama kutoka ngome zao kwa sababu ya shinikizo kutoka kwa vikosi vya usalama katika maeneo ya Kaskazini Mashariki mwa nchi.