Amuua mkewe kwa gurunedi Afrika Kusini

Image caption Polisi wa Afrika Kusini

Polisi nchini Afrika kusini wanamtafuta mwanamme mmoja ambaye analaumiwa kwa kumuua mkewe kwa kutumia gurunedi.

Inadaiwa kuwa wawili hao walikuwa wakijibizana wakati mwananme huyo alimtupia mkewe gurudeni mbili ambapo mojawapo ililipuka.

Mwanamke huyo aliaga dunia saa chache baadaye katika hospitali ya kingsway mjini Durban kutokana na majeraha aliyoyapata kutokana na mlipuko huo ambao pia uliharibu sehemu ya nyumba yao.

Mwanamme huyo anashukiwa kuwa mwanajeshi katika jeshi la Afrika Kusini.

Polisi wa kutegua mabomu walipata moja ya magurunedi hayo ambalo halikuwa limelipuka na kuliondoa eneo hilo.