Wapinga kujitenga mashariki mwa Ukrain

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wapinga kujitenga mashariki mwa Ukrain

Watu wapatao watano wamejeruhiwa katika mapigano kati ya waandamanaji na polisi katika mji mkuu Kiev nchini Ukraine.

Ghasia hizo zimefanyika nje ya bunge wakati mswada unaoruhusu kujitenga kwa eneo la mashariki linalozozaniwa kupitishwa katika awamu ya kwanza.

Mamia ya wanaounga mkono utaifa wanaopinga mswada huo walijaribu kuangusha ukuta unaozunguka bunge na polisi kwa upande wao wakafyatua gesi ya kutoa machozi.

Sheria hiyo inatoa nafasi zaidi kwa Donetsk na Luhansk yanayodhibitiwa na waasi wanaoungwa mkono na Urusi .