Fraizier Glenn ahukumiwa kwa mauaji

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mzee Fraizier Glenn Cross mwenye miaka 74 ahukumiwa kwenda jela kwa mauaji,Marekani

Wanasheria nchini Marekani wamemhukumu kwenda jela Fraizier Glenn mwenye umri wa miaka 74 kwa kosa la mauaji katika shambulio la kituo kimoja cha Wayahudi cha mji wa Kansas.

Imebainika kuwa Glenn aliwaua kwa kuwapiga risasi hadi kufa Wyahudi watatu,April mwakajana kwa madai ya kwamba walikuwa na nguvu na walikuwa na mpango wa kuangamiza watu wenye ngozi nyeupe.

Katika hatua isiyo ya kawaida Glenn Cross muda mfupi baada ya hukumu yake alitoa salaam ya kijeshi yaani salute ya Kinazi wakati wanasheria wakitoka nje ya Mahakama.